Programu hii ndiyo kituo cha amri cha mfumo wako wa Velop na vipanga njia vya Linksys Smart WiFi. Tumia programu ya Linksys mahali popote ambapo una muunganisho wa intaneti ili kuangalia vifaa vilivyounganishwa, kuweka mipangilio ya ufikiaji wa wageni, au kuwazuia watoto wako kwenye mtandao wakati wanapaswa kufanya kazi za nyumbani.
SIFA MUHIMU
• Ufikiaji wa Mbali - Unachohitaji ni mtandao.
• Dashibodi - Takwimu muhimu za WiFi yako kwenye ukurasa mmoja.
• Ufikiaji wa Wageni - Wape marafiki ufikiaji wa mtandao, lakini weka data ya kibinafsi salama.
• Kuweka Kipaumbele kwa Kifaa - Boresha utiririshaji na uchezaji mtandaoni kwa kutoa kipaumbele cha WiFi kwa vifaa vinavyopendelewa.
• Usalama wa Mtandao - Kuwa mwangalifu dhidi ya vitisho vya mtandao na tovuti hasidi ukitumia Linksys Shield.
• Udhibiti wa Wazazi - Himiza tabia nzuri ya watoto kwenye intaneti kwa kusitisha ufikiaji wa mtandao.
Sera ya Faragha: https://www.linksys.com/embed/lswf/en-us/privacy-policy/
Masharti ya Matumizi: https://www.linksys.com/embed/lswf/en-us/terms/
MAHITAJI YA MFUMO*
• Mifumo ya Velop na vipanga njia vya Linksys Smart WiFi. Orodha kamili ya vipanga njia vinavyotumika: http://www.LinksysSmartWiFi.com/cloud/ustatic/mobile/supportedRouters.html
• Akaunti ya mtumiaji (iliyoundwa katika programu au katika http://www.LinksysSmartWiFi.com) iliyounganishwa kwenye bidhaa yako ya Linksys.
• Android 9.0 na zaidi
Laini yetu ya bidhaa ya Velop ina usanidi wa Bluetooth. Katika Android 6 na matoleo mapya zaidi, ni lazima programu ziombe ruhusa za eneo ili kutumia Bluetooth. Hatukusanyi au kutumia maelezo yoyote ya eneo katika programu yetu.
Kwa usaidizi zaidi, tembelea tovuti yetu ya usaidizi katika http://support.linksys.com
Ilisasishwa tarehe
24 Apr 2024