Tafuta, linda, ufute data yote au ucheze sauti kwenye vifaa vyako vya Android vilivyopotea.
Angalia simu, kishikwambi, vipokea sauti vyako vya kichwani na vifuasi vingine kwenye ramani, hata vikiwa viko nje ya mtandao.
Cheza sauti ili utambue mahali kilipo kifaa chako kilichopotea ikiwa kiko karibu.
Ikiwa umepoteza kifaa, unaweza kukilinda au kufuta data yote iliyo kwenye kifaa ukiwa mbali. Unaweza pia kuweka ujumbe maalum utakaoonyeshwa kwenye skrini iliyofungwa ikiwa mtu atakipata kifaa chako.
Data yote ya mahali iliyo katika mtandao wa Tafuta Kifaa Changu imesimbwa kwa njia fiche. Data hii ya mahali haionekani hata kwa Google.
Kanusho
Mtandao wa programu ya Tafuta Kifaa Changu unahitaji mipangilio ya muunganisho wa intaneti na toleo la Android 9 au toleo jipya zaidi.
Inapatikana katika nchi mahususi na kwa watumiaji waliokidhi vigezo vya umri.
Ilisasishwa tarehe
3 Des 2024