Michezo huchangamsha sana ukitumia programu ya Michezo ya Google Play. Gundua mchezo mpya uupendao, kisha ushindane na marafiki zako na ufuatilie mafanikio unayopata. Unavyojua michezo mingi, onyesha ujuzi wako katika maelezo yako ya michezo. Pia, unaweza kuendelea ulipoachia ukitumia kifaa chochote. Cheza na marafiki, popote walipo, katika sehemu moja.
VIPENGELE MUHIMU
• Maelezo ya mchezaji: Unda Kitambulisho maalum cha mchezaji, pata alama za XP na uongeze kiwango kadri unavyoendelea kubobea katika Michezo kwenye Google Play.
• Mafanikio na bao za wanaoongoza: Kamilisha mashindano, pata zawadi, na uzifuatilie ukiwa ndani ya programu. Kisha, ujilinganishe na wachezaji wengine.
• Michezo ya Google Iliyojumuishwa Ndani: Cheza PAC-MAN, Solitaire, Snake, na Cricket — hata ukiwa nje ya mtandao.
• Ukumbi wa michezo: Pata mchezo unaokupendeza katika sehemu ya mikusanyiko Mipya, Inayovuma na Chaguo za Wahariri.
• Kurekodi uchezaji*: Rekodi na ushiriki kwa urahisi matukio bora ya mchezo wako kutoka michezo uipendayo ya vifaa vya mkononi.
* Inapatikana tu katika baadhi ya nchi
Ilisasishwa tarehe
10 Des 2024