Umeshawahi kutaka kuwa msimamizi wa uwanja wa ndege na ufanye kazi uwanja wa ndege? kama ni hivyo app hii itakupeleka kwenye uvumbuzi mahususi! Ingia ndani ya uwanja wa ndege na ujiandae kuruka na ndege yenye kiwango cha juu. Vumbua kila kona ya uwanja wa ndege na uwe tayari kusafiri kwaajili ya likizo yako! Onyesha ujuzi wako kwenye ubunifu kwa kusimulia hadithi na kuigiza.
Hivi utavipata ndani ya app hii ?
Eneo la Maduka Yasiyolipiwa Kodi
Fanya manunuzi kama upendavyo moyo wako ndani ya eneo la duka lisilolipiwa kodi ndani ya uwanja wa ndege.Cheza michezo ya kuvaa ndani ya uwanja wa ndege au kujifanya kuwa mfanyakazi wa ndege ndani ya michezo hii ya ndege. Nunua vitu kutoka kwenye mashine za uuzaji na ule vyakula vitamu pia! ni mwanzo mzuri kwaajili ya mapumziko.
Uhamiaji na Eneo la Ulinzi
Hakikisha uwanja wa ndege unakuwa salama kwa kumkagua kila abiria. Hakikisha hakuna kitu cha hatari kinaingizwa kwenye ndege. Kamilisha taratibu zote za kuingia ikiwemo mizigo na ruhusa ya kuingia. Ni sawa na uwanja wa ndege halisi unavyofanya kazi!
Ndege
Pindi taratibu za kuingia zikikamilika, sasa ni muda wa kuingia kwenye ndege! Onja maisha ya wanaoruka kwa kusafiri daraja la biashara pia daraja la chini ndani ya ndege. Kuwa kiongozi wa ndege na uwape huduma nzuri wasafiri wako.
Wasifu:
Waigizaji wapya wakiwemo wafanyakazi wa ndani ya ndege, kiongozi wa uwanja wa ndege na abiria,
Vitu vingi sana vya kuchezea. Ni burudani kutengeneza hadithi yako mwenyewe ndani ya app hii!
Gusa, kokota na uvumbue kila kitu na uone kinachotokea!
Ndege hii na uwanja wa ndege upo salama na Bila matangazo!
Imetengenezwa kwaajili ya watoto wa umri wa miaka 6-8, ila kila mtu ataburudika kuichezea app hii.
Upo tayari kuanza sikukuu yako ya uvumbuzi? Anza sasa kwa kupakua app hii! Safari njema️
Ilisasishwa tarehe
18 Des 2024