Mnadhifishaji

· Lindhardt og Ringhof
3,0
2 mnenji
E-knjiga
120
Strani
Ocene in mnenja niso preverjeni. Več o tem

O tej e-knjigi

Bertram na marafiki zake watatu wameanzisha genge ndogo la majambazi linaloitwa The Hawks. Anaishi peke yake na mama yake, anayefanya kazi kama mhudumu hotelini. Hamkumbuki baba yake sana, kwa kuwa alikamatwa kwa makosa ya mauaji na kufungwa kifungo cha maisha Bertram akiwa umri wa miaka misaba pekee. Siku moja, Bertram aliiba jaketi ya ngozi ya bei ghali yenye chapa ya "Schott Made in USA" kutoka kwa mkahawa, ambayo ilimletea matokeo mabaya sana, na si kwa Bertram pekee. Rolando Benito, mpelelezi katika Mamlaka ya Malalamiko ya Polisi, na wenzi wake walitumwa ili kuwauliza maswali maafisa wawili wa polisi. Mlinzi wa gereza alikuwa ameruka nje ya dirisha lake katika ghorofa ya nne, huku maafisa hao wawili wakimvuta, baada ya malalamiko ya kelele nyingi iliokuwa ukitoka kwenye nyumba yake. Kwa kuwa mlinzi huyo wa gereza alikuwa baba ya rafiki wa shule wa mjukuu wa Rolando, yeye husikia uvumi kwamba mfungwa alikufa ndani ya gereza ambalo mtu huyo alikuwa akifanya kazi, na kwamba mlinzi wa gereza alihisi ametishwa na kuteswa. Kwa hivyo mwishowe hii si kesi ya kujitoa uhai? Anne Larsen, mwanahabari wa TV2 East Jutland, ako pia katika kesi hii. Kila mtu anaonekana kuwa na uhusiano na mfungwa mmoja, muuaji Patrick Asp, aliyeua mtoto wake mwenyewe mchanga na ni mfungwa katika gereza ambalo mlinzi huyu wa gereza alikuwa akifanya kazi. Vifo hivi vya kutatanisha vikiendelea kuongezeka, na hakimu wa Mahakama Makuu akipotea bila kugunduliwa, Rolando Benito na Anne Larsen wanaunganika wakitafuta uhusiano. Uhusiano huo unapatikana kuwa ni Bertram na wizi wa jaketi, na sasa Anne ako hatarini pia. Inger Gammelgaard Madsen (b. 1960) ni mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Inger Gammelgaard Madsen ana uasilia wa kisomo cha uchoraji wa vielelezo. Alianza kuandika hadithi zinazohusu uhalifu "Dukkebarnet" katika mwaka wa 2008. Baada ya kitabu hiki, ameandika vitabu vingine kadhaa vinavyohusu uhalifu. Baadhi ya vitabu hivi ni "Drab efter begæring" (2009), "Slangers gift" (2014), "Dommer og bøddel" (2015) na "Blodregn" (2016).

Ocene in mnenja

3,0
2 mnenji

Ocenite to e-knjigo

Povejte nam svoje mnenje.

Informacije o branju

Pametni telefoni in tablični računalniki
Namestite aplikacijo Knjige Google Play za Android in iPad/iPhone. Samodejno se sinhronizira z računom in kjer koli omogoča branje s povezavo ali brez nje.
Prenosni in namizni računalniki
Poslušate lahko zvočne knjige, ki ste jih kupili v Googlu Play v brskalniku računalnika.
Bralniki e-knjig in druge naprave
Če želite brati v napravah, ki imajo zaslone z e-črnilom, kot so e-bralniki Kobo, morate prenesti datoteko in jo kopirati v napravo. Podrobna navodila za prenos datotek v podprte bralnike e-knjig najdete v centru za pomoč.