Tumia kamera yako kukuza maandishi madogo, kuona maelezo ya vitu au kuvuta karibu maandishi yaliyo mbali kama vile alama za barabarani au menyu za mikahawa nyuma ya kaunta ya huduma. Tafuta maneno ndani ya picha unazopiga ili upate unachohitaji kwenye menyu, ubao wa wakati wa kuondoka au kitu chochote kilicho na maandishi. Tumia madoido yanayoonekana ili maandishi yenye utofautishaji mdogo yaonekane zaidi. Katika mazingira ya mwangaza hafifu, ung'aavu hurekebishwa kiotomatiki. Unaweza pia kupiga picha na kuvuta karibu kadri unavyohitaji.
Anza:
1. Pakua kipengele cha Kikuzaji kwenye Duka la Google Play.
2. (Si lazima) Weka mipangilio ya Kikuzaji ili ufungue kwa urahisi kupitia kipengele cha Kugusa haraka:
a. Fungua programu ya Mipangilio ya simu yako.
b. Nenda kwenye Mfumo > Ishara > Kugusa haraka.
c. Washa Tumia kipengele cha Kugusa haraka.
d. Chagua fungua programu. Karibu na "Fungua programu," gusa Mipangilio. Kisha chagua Kikuzaji.
e. Ili ufungue Kikuzaji, gusa mara mbili nyuma ya simu yako.
Kikuzaji kinahitaji Pixel 5 au muundo mpya.
Ilisasishwa tarehe
18 Nov 2024