Google Maps Go ni toleo jepesi la Programu ya Wavuti ya Kisasa ya programu halisi ya Ramani za Google.
Toleo hili linahitaji Chrome (ikiwa hungependa kusakinisha Chrome, tafadhali tumia www.google.com/maps kwenye kivinjari chako badala yake).
Ikilinganishwa na toleo kamili la Ramani za Google, Google Maps Go huchukua nafasi ndogo zaidi kwenye kifaa chako na huendeshwa bila tatizo katika vifaa vyenye nafasi ndogo ya hifadhi na kwenye mitandao isiyotegemeka bila kuathiri kasi ya kukuonyesha mahali ulipo, taarifa za trafiki kwa wakati halisi, maelekezo, na maelezo ya usafiri wa umma wa treni na basi. Unaweza pia kutafuta na kupata maelezo kuhusu mamilioni ya maeneo kama vile nambari za simu na anwani.
• Tafuta njia ya haraka zaidi inayojumuisha usafiri wa bodaboda, treni, basi, teksi, kutembea, na vivuko vya feri
• Safiri mjini kwa basi au treni ukitumia ratiba za usafiri wa umma za moja kwa moja
• Pata maelekezo ya hatua kwa hatua pamoja na chaguo la kukagua kwanza njia, ili kukusaidia kupanga safari zako mapema
• Wasili unakoenda haraka kwa kutumia taarifa za trafiki na ramani za trafiki
• Gundua na utembelee maeneo mapya
• Tafuta na upate mikahawa, biashara na maeneo mengine ya karibu
• Baini maeneo ya kutembelea kwa kuangalia maoni ya wateja na picha za vyakula
• Pata anwani na nambari ya simu ya mahali fulani
• Hifadhi kwenye kifaa chako cha mkononi maeneo unayotaka kutembelea mara kwa mara, na uyapate haraka baadaye
• Inapatikana kwa zaidi ya lugha 70
• Ramani za kina na sahihi (ikijumuisha setilaiti na mandhari) katika nchi na maeneo 200
• Taarifa za usafiri wa umma katika zaidi ya miji 20,000
• Maelezo ya kina ya biashara kuhusu zaidi ya maeneo milioni 100
____
Jisajili ufanye jaribio la beta: https://goo.gl/pvdYqQ
Ilisasishwa tarehe
24 Okt 2023